ads slot

Latest Posts:

Kajala Amrushia Ujumbe Wema Sepetu Ambae Amekuwa Mgumu Kusamehe “Love will save us”

KAJALA Masanja ambaye ana bifu na aliyekuwa shosti wake mkubwa, Wema Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumpa rafiki yake huyo wa zamani ujumbe unaoashiria upendo kwa kuvaa gauni lenye maandishi yaliyosomeka “Love will save us” yakimaanisha upendo utatuokoa.

‘Katukio’ hako kalinaswa na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar kulikokuwa na onesho la Mrs.
Mabeste Charity (mke wa msanii Mabeste) ambayo ilikusanya wasanii wengi wakiwemo Kajala na Wema.

Baada ya mwandishi wetu kushuhudia ujumbe huo mgongoni mwa Kajala huku marafiki zake wakidai ni maalum kwa Wema ambaye amekuwa mzito kusamehe ugomvi wao, alimuuliza kama amemlenga Wema au ni vazi tu alivaa?
“Jamani mimi nimevaa tu, sikumkusudia mtu,” alisema Kajala.Wema na Kajala wamekuwa kwenye bifu la kuchukuliana bwana na bado hawajafikia muafaka.

GPL
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment