ads slot

Latest Posts:

Uongozi wa chuo kikuu cha sabastian umeshindwa kutoa jibu la kuridhisha

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sabastian Koloa SEKOMU, Jijini Tanga umeshindwa kutoa majibu ya kuridhisha kutokana na ombi ambalo limetolewa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Chuo hapo kudai kuitwa Magaidi
Hivi karibuni Jumuiya hiyo iliitaka Uongozi wa Chuo cha SEKOMU kukomesha kauli zinazotolewa dhidi ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo hicho kuwa ni Magaidi, na kuwapa muda wa kutekeleza Ibada ya Siku ya Ijumaa.

Kutokana na ombi hilo Uongozi wa Chuo hicho, uliitisha Kikao cha Wanafunzi wote jana, na kushindwa kutoa majibu ya malalamiko ya Wanafunzi hao wa Kiislamu, na  kutoa majibu kupitia barua ambayo haikufafanua malalamiko hayo.

Akizungumza na Dira ya Habari,  Amiri Mstaafu wa Jumuiya  ya Wanafunzi wa Kiislamu Chuoni hapo, Ally Ramadhani Ally, ameweka bayana majibu yaliyoandikwa katika barua hiyo.

Hayo yanajiri baada ya hivi karibu Jeshi la Polisi kuwakamata Wanafunzi Watatu kwa kupewa taarifa na Uongozi wa Chuo, ambacho kipo Kijiji cha Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kuwa Wanafunzi hao wanahatarisha amani ya Chuo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment